Katibu Mkuu Dkt. Jane Kere Imbunya Azungumzia Utendakazi Serikalini
Katibu Mkuu Dkt. Jane Kere Imbunya Azungumzia Utendakazi Serikalini
Katibu Mkuu wa Utumishi wa Umma, Dkt. Jane Kere Imbunya, tarehe mosi alishiriki mahojiano katika kipindi cha Jambo Kenya cha Redio Citizen. Katika mahojiano hayo, alitumia fursa hiyo kuangazia masuala muhimu yanayohusu idara yake pamoja na utendakazi wa serikali kwa jumla.
Miongoni mwa masuala aliyojadili ni pamoja na mageuzi yanayoendelea, uboreshaji wa utendakazi, na mipango maalum iliyowekwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za serikali kwa wakati na kwa uwazi.